Chuo cha Theolojia Utengule
Chuo cha Theolojia
Utengule kilianzishwa mwaka 1954, kwa misingi ya Chuo Kikuu cha Kibiblia cha
Moravian, kilichoanzishwa na wamisionari wa Kijerumani mwishoni mwa karne ya
19. Chuo cha Theolojia Utengule kipo katika eneo la utulivu na amani,
kimezungukwa na mazingira mazuri ya Utengule, umbali wa kilomita 7 nje ya
Mbalizi.
Tunatoa kozi
zifuatazo:
-
Cheti katika Theolojia - (Miaka 3)
Cheti kwa Wainjilisti / Mafunzo ya Biblia - (Miaka 2)
Cheti katika muziki (kozi maalum)
Kozi ya diploma inatarajiwa kuanza mwezi Agosti 2019
Mwezi Machi 2019,
takriban wanafunzi 70 wamesajiliwa katika chuo chetu. Wanawake wanakaribishwa
kuomba zaidi, kuwaunga mkono wanafunzi wa kike. Pia tunawahimiza wanafunzi wa
mashirika mengine kuomba. Chuo hiki si kwa ajili ya
Wakristo wa kanisa la Moravian tu.
Vifaa
Tunatoa vifaa
mbalimbali vyenye lengo la kuboresha hali ya usomaji katika chuo kikuu. Kuna
maktaba, iliyo na vitabu takriban 2000 kusaidia ufundishaji na ujifunzaji. Kuna
maabara ya kompyuta, pia kuna mabweni ya wanaume na wanawake yanayokuruhusu
kukaa kwenye eneo la chuo.
Ukweli ni kwamba chuo kiko kwenye eneo kubwa (zaidi ya ekari 15) linalotuwezesha kuendesha miradi mingi ya kuzalisha mapato. Chuo kinafanya shughuli zake za kilimo, wakiwamo ng'ombe, nguruwe na mashamba ya mahindi, maharage, ndizi na mboga. Zaidi ya hayo, tuna bwawa letu la samaki, ambapo tunafuga samaki kama chanzo bora cha protini.
Wafanyakazi
Mkuu | Makamu Mkuu | Mataaluma Mkuu |
Rev. Amos Mwampamba | Rev. Sifael Mwashibanda | Rev. Ezekia Petro Majani |
Lengo
Neno la Mungu kama
lilivyoandikwa katika Agano la Kale na
Agano Jipya kuwa msingi wa mafundisho yote ya kitheolojia.
Mtazamo
Kuwa mojawapo ya
vyuo bora zaidi cha kumboresha mwanafunzi katika nyanja mbalimbali za
kitaaluma, mafunzo, utafiti wa kitheolojia na uwezo wa ushauri na pia mfano
bora kwa jamii yenye maadili mema.
Motto
Kumjua Mungu na neno lake katika Yesu Kristo.
Malengo
1. Kuwafundisha wachungaji, wainjilisti, walimu wa mitaa, wakufunzi wa Biblia, wakufunzi wa muziki na wahudumu wengine wa kanisa.
2. Kuboresha msingi wa mafunzo ya Theolojia
3. Kuwafundisha
wahudumu wa kanisa elimu ya kidunia (kama vile masuala ya kijamii).
Chuo
cha Theolojia Utengule
S.L.P. 185
Utengule
Tanzania
Simu: +255 755 148514