MVTC – Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi Moravian
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Moravian (MVTC) kilianzishwa mwaka 2000 jijini Mbeya, Old Forest, Kadege. Kimesajiliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Lengo la shule ni kuandaa kizazi cha vijana wa Kitanzania, bila kujali jinsia wala dini, kupata elimu zaidi, elimu ya kiufundi kwa kiwango cha kitaifa na ajira endelevu. Ndiyo maana, tunafundisha pia ujuzi wa maisha na ujasiriamali katika kozi zetu zote. Chuo kina uwezo wa wanafunzi 450, kwa sasa wanafunzi 400 wamesajiliwa (2019).
Tunatoa kozi za muda mrefu katika taaluma zifuatazo:
- Useremala na Uundaji
- Ufundi wa magari
- Ufundi umeme wa magari
- Ufundi umeme wa majumbani (pia nishati ya jua kwa wanafunzi wa ngazi ya juu) (DEI)
- Kozi ya uhadhiri
- Upishi
- Ushonaji na ubunifu wa mavazi
Kozi hizi
zinatolewa kwa kipindi cha miaka miwili. Tunaendesha Mitihani ya Taifa ya
Msingi (National Based Exams) na Tathmini ya Msingi ya Uwezo (Competence Based
Assessments) katika chuo chetu na tunawaandaa wanafunzi wetu kwa Mitihani ya
Taifa. Kila mwanafunzi anapata zana za msingi anapomaliza masomo yake ili aanze
biashara yake mwenyewe (kama vile mashine ya kushonea kwa washonaji).
MVTC pia hutoa kozi za muda mfupi katika taaluma zifuatazo:
- Kozi ya mafunzo ya kompyuta (muda unategemea programu)
- Kozi ya udereva (wiki 5)
- Kozi ya kiingereza (miezi 3)
- Uendeshaji wa hoteli na Utalii (miezi 3 hadi 9)
- Ushonaji (miezi 6)
- Ufundi umeme wa majumbani (miezi 6)
- Ufundi wa magari (miezi 6)
- Ufundi umeme wa magari (vyombo vya moto) (miezi 6)
- Useremala na
uundaji (miezi 6)
Vifaa
Tunatoa vifaa
mbalimbali ili kuboresha uzoefu wa kujifunza katika kituo chetu. Kuna mabweni
ya wavulana yenye uwezo wa wanafunzi wapatao 50, kwenye eneo la chuo. Pia kuna
mabweni ya wasichana yenye uwezo wa wanafunzi 120.
Chuo kina maabara
mbili za kompyuta zenye kompyuta zipatazo 50, mtandao wa intaneti (wireless) na
vifaa vingine muhimu vinavyotuwezesha kutoa mafunzo ya kitaaluma katika
programu ya kompyuta. Kuna jiko lililokamilika kwa ajili ya kozi ya upishi na
gereji kwa mafundi wa magari na kozi za ufundi wa umeme. Zaidi ya hayo, kuna
maktaba yenye vitabu na kompyuta inayotumiwa na wanafunzi. Pia kuna mtandao wa
intaneti kwenye maktaba.
Pia, Chuo cha
Ufundi cha Moravian kina vitengo viwili vya uzalishaji. Kitengo cha useremala
hutengeneza samani (kwa ajili ya ofisi, shule, mabweni na kampuni binafsi).
Pia, kuna waajiriwa tisa wa vitengo vya utengenezaji wa majeneza, mizinga ya
nyuki na fanicha mbalimbali. Kitengo cha ushonaji kimejikita katika ushonaji wa sare ( za wanafunzi, wachungaji na siku za mahafali),
pia nguo binafsi
Mkuu - Gad Lwinga | Mratibu wa Mafunzo - Shadrak Gondwe | Mhasibu - Barnabas Mwang'onda | Mhasibu Msaidizi - Famuel Mwandeko |
Mtazamo
1. Vijana bila kujali jinsia wanawezeshwa kuja kujiajiri.
2. MVTC kinajiendesha kwa rasilimali zake na msaada kutoka kanisani.
3. Kampuni ndogo
ndogo za kibiashara zilizopo zinawezeshwa
Mawasiliano
MVTC - Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi Moravian
S.L.P. 152
Mbeya
Tanzania
Barua Pepe: mvtcmbeya@gmail.com
Simu: +255 025 2503272
+255 755 766 862