Matukio Yajayo

  • Mbaraka wa Wachungaji katika ushirika wa Iyunga   Oktoba, 2021
  • ziara ya Mch. Dk. Jochen Tolk Oktoba, 2021

Matukio ya hivi karibuni

  • Mbaraka wa Wachungaji katika Ushirika wa Iyunga wachungaji, wainjilisti na ndugu watakuwa na  mfungo wao katika Hostel ya Jimbo  kuanzia 19- 24 Oktoba, 2021 na mbaraka kufanyika katika Ushirika wa Iyunga. 
  •  Hivyo  wataobarikiwa kuwa mashemasi watakuwa 28  na wataobarikiwa kuwa makasisi watakuwa wachungaji 32.
  • Ibada ya Mbaraka wa Wachungaji itafanyika katika ushirika wa Iyunga tarehe   24/10/2021 itaongozwa na Mchg. Willey Mwasile  na Askofu Dkt. Alinikisa F. Cheyo akiwawekea mikono.
Mashemasi wakibarikiwa
  

  • Ndoa ya Askofu Alinikisa F. Cheyo,  wa Kanisa la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini-Magharibi, tarehe 21 Agosti 2021 katika ushirika wa Yerusalemu, Mbeya. Ikumbukwe Jimbo la Kusini Magharibi lilikumbwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na mke wa kwanza wa Askofu na mazishi kufanyika tarehe 13/06/2019 katika Ushirika wa Yerusalemu.
  • Mungu akasikia maombi ya waumini wa Kanisa la Moravian kwa ajili ya Baba Askofu kuwa na Mwenza. Bwana abarikiwe sana 
Ziara ya Mch. Dk. Jochen Tolk mfadhili wa vyuo vya Ufundi Chunya na Ilindi itakuwa mwezi Oktoba 2021. hivyo atakuja kukagua miradi anayofadhili katika Jimbo letu. Mch. Tolk anakumbuka jinsi alivyofanya kazi katika jimbo hili la Kusini Magharibi.
Kila mwaka anajitahidi kutembelea Chunya, Ilindi na hata Jimbo la Kusini. Tunamwombea kwa Mungu asafiri salama katika safari yake.

 
Kuagwa kwa Ndugu Etienne Jenni MVTC na Makao Makuu
KMT-JKM iliandaa tafrija fupi kwa ajili ya kumwaga ndugu Etienne Jenni aliyefanya nasi kama mtengenezaji wa tovuti ya kanisa na kompyuta. Alianza kufanya kazi Novemba 3, 2018 hadi Julai 1, 2019. Tafrija zilifanyika Chuo cha Ufundi Moravian tarehe 25.06.2019 na Makao Makuu tarehe 27.06.2019
KMT-JKM inamtakia safari njema kurudi kwao Uswissi.
25.06.2019 katika Chuo cha Ufundi Moravian
27.06.2019 katika Makao Makuu Jacaranda
Kozi ya Ufumaji masweta na Ushonaji

Darasa la awamu ya saba limefanya mahafali yake leo tarehe 29 Juni,2019 hapa Jacaranda. Darasa linaendeshwa na Idara ya Umoja wa Wanawake na Watoto na kufadhiliwa na Mission 21.
Wanafunzi wa darasa hili walianza 24 na mwisho wa mafunzo yao walifanikiwa kumaliza wanafunzi 19.
Hotuba ya wahitimu  29.06.2019wahitimu wa awamu ya sita

TANZIA
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi limepoteza  wachungaji wengi mwaka huu wa 2021kama vile Mch. Owdencalm Mpayo, Mch. Faraja A. Cheyo (misioni Iringa),

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe.

MATUKIO YA MBARAKA NA SINODI YA KATIBA
mbaraka wa wachungaji ulifanyika katika Ushirika wa Mabatini tarehe 03/11/2019. kabla ya mbaraka huo wachungaji, ndugu na wainjiisti walikuwa na mfungo wa siku nne (4) kuanzia tarehe 29/10/2019 hadi tarehe 02/11/2019.

Mfungo uliongozwa na Askofu Dkt. Alinikisa Cheyo na viongozi wa Kamati Tendaji. waliopata mbaraka wa Ushemasi walikuwa watatu (03) kati yao akiwepo mwanamke mmoja. waliopata mbaraka wa Ukasisi walikuwa wachungaji wanane (08).

Ibada ya mbaraka wa wachungaji iliongozwa na mwenyekiti wa Jimbo Mchg. Zakaria Sichone na Askofu Dkt. Alinikisa Cheyo aliwawekea mikono waliobarikiwa.
Kiswahili