Urafiki na Nchi za nje

URAFIKI NA MISSION 21
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi limekuwa na urafiki na shirika la Mission 21 yenye Makao yake huko Basel- Uswissi.
Shirika hili linaendelea kulisaidia jimbo letu katika mambo mengi kwa mfano Watoto ya Yatima na wanaoishi katika Mazingira Magumu, Maswala ya kupunguza maambukizi ya VVU, kuboresha maisha ya watumishi katika Jimbo (Capacity Building), Kilimo na Elimu. Hizi ni baaadhi tu ya shughuli zinazofanywa na shirika hili.

Makao makuu ya Mission 21 yapo ofisi kuu Jacaranda ya kiongozwa na Adrianne Sweetman pia Adrianne anasaidiwa na Israel Mwakilasa.
Uhusiano kati ya Jimbo letu na shirika hili ni mzuri sana hivyo Mchg. Johannes Klemm kama mwangalizi wa shughuli za Mission 21 Africa ametutembelea sana na Makamu Mwenyekiti wa KMTJKM Mchg. Willey Mwasile amealikwa kwenda kutoa mada inayohusu Ukatili wa kijinsia katika Jamii. Makamu Mwenyekiti ametuwakilisha vizuri kiasi kwamba marafiki wamefurahi sana kwa kazi waifanyayo katika Jimbo letu (KMTJKM).

Makamu Mwenyekiti Mchg. Willey Mwasile akiwa Uswissi pamoja na baadhi ya marafiki wa Mission 21 huko Basel

Kiswahili