Taasisi za Elimu
Katika utume wetu wa kuleta maendeleo katika jumuiya na maeneo yaliyotuzunguka, moja ya malengo makuu ni kutoa elimu bora iliyo nafuu kwa kila mtu. Kwa sababu hiyo, Kanisa la Moravian Tanzania – Jimbo la Kusini – Magharibi linaendesha taasisi kadhaa za elimu katika Mbeya mjini na mikoa inayoizunguka. Kwa taarifa zaidi kuhusu taasisi hizo, bonyeza linki za chini.
Chuo cha Mafunzo
ya Ufundi cha Moravian (MVTC) kinapatikana jijini Mbeya, Old forest, Kadege.
Chuo kimesajiliwa na Mamlaka ya Mafunzo ya Elimu ya Ufundi (VETA) na kinatoa
kozi za muda mrefu za miaka miwili katika taaluma saba (7) mbali mbali na kozi fupi
nyingi.
Vyuo vingine:
- Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Chunya
- Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Ilindi
- Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Sadock Simwanza
Shule ya sekondari ya Mbozi, inapatikana katika mandhari nzuri pembeni mwa mji Mbozi, ni mojawapo ya shule binafsi kongwe mkoani Mbeya. Inatoa mafunzo katika vidato vyote (Kidato cha 1-6).
Chuo cha Ualimu
Mbeya Moravian
Baada ya serikali
kuzindua kampeni "shule moja kwa kila kijiji" mwaka 2000, shule
nyingi zilijengwa. Kwa bahati mbaya, idadi ya walimu haikukidhi mahitaji. Kulikuwa
na ongezeko kubwa la mahitaji ya walimu wenye sifa. Kwa kukabiliana na hitaji
hili, Chuo cha Walimu cha Kanisa la Moravian kilifunguliwa katika jiji la Mbeya
mwaka 2009.
Chuo cha Theolojia Utengule kipo katika eneo la utulivu na amani, kimezungukwa na mazingira mazuri ya Utengule, iliyo umbali wa kilomita 7 nje ya Mbalizi. Chuo kinatoa kozi ya cheti katika Theolojia, kozi za kiinjilisti (Mafunzo ya biblia) na kozi ya cheti katika muziki.
Taasisi ya Afya Yohana Wavenza - Yohana Wavenza Health Institute
Taasisi ya afya ya
Yohanna Wavenza iko Mbozi kwenye kambi ya Hospitali ya Mbozi Mission, kilomita
7 kutoka barabara kuu ya Mbeya-Tunduma. Inatoa Diploma ya uuguzi na ukunga
(miaka 3).