Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Sadock Simwanza

Chuo cha VETA Sadock Simwanza, kipo pembeni ya Tunduma, kilianzishwa mwaka 2017. Chuo kipo umbali wa kilomita 45 toka mji mdogo wa Tunduma katika barabara iendayo Sumbawanga. Kwa sasa, zaidi ya wanafunzi 20 wamesajiliwa katika chuo chetu na walimu wapatao saba wanafanya kazi hapo. Chuo kinapokea wanafunzi wa bweni na kutwa. Chuo kina uwezo wakupokea wanafunzi mia (100) kwa wakati mmoja.

Sifa za Kujiunga na Chuo
1. Mwanafunzi aliyehitimu elimu ya msingi na kuendelea
2.  Kwa kozi ya Hoteli na Utalii awe amehitimu kidato cha nne
3. 

Tunatoa kozi zifuatazo:

  • Ushonaji na Ubunifu wa nguo au mavazi (miaka 2)
  • Ufundi umeme wa majumbani (miaka 2)
  • Mafunzo ya kompyuta na matengenezo (miaka 2)
  • Mafunzo ya Hoteli na Utalii (miaka 2)
  • Mafunzo ya Uhazili (miaka 2)

Zaidi ya hayo, ujuzi wa msingi katika kilimo unafundishwa miongoni mwa kozi zote.

Vifaa

Tuna vifaa mbalimbali vinavyochangia mazingira bora ya kujifunza. Miongoni mwa hivyo, ni darasa maalam lenye vifaa vya kushonea, maabara ya kompyuta yenye mtandao wa intaneti, uhazili, hoteli  na utalii  na bweni la wanafunzi wa kike. Pia, kuna maji na umeme.


Utawala

MkuuMakamu MkuuMhasibu
Rev. Raison Kibona
Selemani MembaFaraja Isaya

Motto wa Shule

"We light up your way to success."

Mawasiliano

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Sadock Simwanza

S.L.P. 43
Tunduma 
Tanzania

Barua Pepe:    sadocksimwanzavtc@gmail.com
Simu:     +255 752 221 317

Kiswahili