Shule ya Sekondari Mbozi
Iko pembeni ya
Mbozi katika eneo zuri, Shule ya sekondari ya Mbozi (High School) inafundisha
ngazi zote (Kidato cha 1 - 6). Imegawanywa katika madarasa kumi na nne.
Wanafunzi 234 (2019) wanapata mafunzo bora na kila mada hufundishwa kwa
Kiingereza isipokuwa somo la Kiswahili. Wanafunzi wa kike ni asilimia zipatazo
50.
Mtazamo
Shule ya sekondari bora yenye kutoa elimu bora kwa wanafunzi na wanajamii wanaoishi pamoja kwa upendo, amani na maadili mema.
Lengo
Kutoa elimu bora
kwa wanafunzi wote na wanajamii katika shule ya sekondari iliyoanzishwa vizuri
yenye miundo mbinu iliyokamilika na
huduma za kijamii.
Motto wa Shule
Nidhamu na Elimu
ni misingi ya maendeleo.
Malazi
Shule hutoa huduma
ya malazi kwa wavulana na wasichana. Bweni la wasichana lipo shuleni na
linamudu wanafunzi wapatao 450.
Bweni la wavulana
pia linapatikana kwenye eneo la shule
linalomudu wanafunzi wapatao 300.
Tunatoa vifaa
mbalimbali ili kuboresha hali ya kusoma shuleni kwetu. Miongoni mwa vifaa hivyo
ni maabara ya kompyuta, maktaba, maabara ya fizikia, maabara ya kemia,
baiolojia na zahanati.
Elia Msyaliha - Mkuu wa shule | Sijali Benson Mpesya - Makamu Mkuu wa shule | Tuosi Mwamengo - Mtaaluma Mkuu |
Raphael Watson - Mtaaluma msaidizi | Omary Sinkonde - Mwalimu wa nidhamu | Mussa Anyimike - Mhasibu wa shule
|
Pakua fomu yetu ya
kujiunga hapa na umpe mtoto wako fursa ya kusoma katika Shule ya Sekondari Mbozi!
Mawasiliano
Shule ya Sekondari Mbozi
S.L.P. 341
Mbozi-Songwe
Tanzania
Barua Pepe: mbosec@yahoo.com
Simu: +255 754 203 749