Taasisi ya afya ya Yohana Wavenza
Taasisi ya afya ya
Yohana Wavenza ni chuo cha uuguzi ambacho kilianzishwa mwaka 2011. Kinapatikana
kwenye eneo la Hospitali ya Mbozi misheni. Mafunzo ya kwanza yalianza mwezi
Septemba 2011 na wanafunzi wapatao 85. Leo, zaidi ya wanafunzi 180 wamejiunga na taasisi yetu na walimu 7 hutoa mafunzo yenye ubora. Tunatoa
kozi ya diploma ya uuguzi na ukunga kwa miaka mitatu.
Vifaa
Tunatoa vifaa
mbalimbali vyenye lengo la kuhakikisha mazingira
bora ya kujifunzia wanafunzi wetu. Kama vile, chumba cha kompyuta, maktaba na
mabweni kwa wanafunzi wa kiume na wa kike.
Mtazamo
Taasisi ya afya ya
Yohana Wavenza Mbozi imejidhatiti kutoa huduma za afya kwa kutoa elimu bora ya
uuguzi, ugunduzi na mafunzo bora ya vitendo.
Lengo
Kutoa mafunzo bora
kupitia wafanyakazi wenye uwezo na wenye kujituma wanaotumia mbinu zinazofaa
katika mazingira mazuri.
Maadili
- Ubora wa mafunzo na huduma za afya
- Ufanisi na utendaji wa shughuli
- Mazingira ya kiutendaji
- Huduma nzuri kwa wateja
Vivutio kutoka
kwenye moja ya sherehe za kuhitimu
Mkuu | Makamu Mkuu |
Vitalis Rizick Magehema | Mediatrix Mwanjee |
Mawasiliano
Taasisi
ya afya ya Yohana Wavenza
S.L.P. 91
Mbozi-Songwe
Tanzania
Barua Pepe: yohanawavenzahealth@gmail.com