Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Chunya

Chuo cha Ufundi Chunya kilianzishwa mwaka 2014, kwa sasa hutoa elimu kwa wanafunzi zaidi ya 30. Tunatoa kozi za ushonaji na ubunifu wa nguo / mavazi kwa miaka miwili kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kwa wanafunzi wenye nia ya kukaa chuoni, tuna bweni letu lenye nafasi kwa wanafunzi 36.

Faida maalum ya kujifunza katika chuo chetu ni kwamba wanafunzi wetu wote hupewa mashine zao za kushonea na vifaa vingine muhimu siku ya mahafali. Hii inawawezesha kuanzisha biashara zao wenyewe na kujitegemea kiuchumi, mara tu wanapomaliza kozi yao!


Baadhi ya vivutio vya mahafali mwaka 2018:

Mawasiliano

Magreth Chungu
Simu: +255 766 434 591

Kiswahili