Sisi Ni Nani

Kanisa la Moravian la Tanzania ni miliki ya Kanisa la Moravian ulimwenguni, kanisa la Kikristo la kiprotestanti . Kanisa lilianza katika Jamhuri ya sasa ya Kicheki (Czech) mwaka 1457 na kiongozi John Hus. Limeenea mahali pengi duniani, ikiwemo Tanzania - lilianzishwa mwishoni mwa karne ya 19.

Kanisa la Moravian Tanzania limegawanyika katika majimbo 7 yanayojitegemea, nchini kote. Makao makuu ya kanisa la Jimbo la Kusini-Magharibi (MCT-SWP) yako Mbeya, jiji la tano kwa ukubwa Tanzania. Ushawishi wake unafikia wilaya tatu za utume: Mbeya, Mbalizi, na Chunya. Zaidi ya hayo, jimbo linasimamia maeneo mawili ya utume, ambayo ni Iringa na Mbozi. Kanisa lina shirika 133, wachungaji 300, na waumini 215,000 (kwa mwaka 2019).

Mtazamo

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini-Magharibi linalenga kumjua Mungu vyema na kuwa na uhusiano mkubwa na Mungu. Yeye ndiye anayetutimizia mahitaji yetu ya kiroho, kimwili na kijamii. Kanisa la Moravian limejikita kumtumikia Mungu na kuwa kioo cha jamii.

Lengo

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi lina lengo la kueneza Neno la Mungu. Kanisa, kwa kusikiliza mahitaji ya waumini wake, na kushughulikia masuala ya jamii, kanisa linafanya haya, kwa kutumia mikakati endelevu kuboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jumuiya kupitia miradi ya elimu, afya, mazingira na vyombo vya habari.


Maadili ya msingi

  1. Mwenendo mzuri na tabia njema katika huduma
  2. Wafanyakazi wenye sifa nzuri zinazotambuliwa na Serikali
  3. Uaminifu na uwajibikaji
  4. Ushirikiano na kuheshimiana
  5. Umoja kupitia maadili ya kibiblia
  6. Ubora wa hali ya juu na ufanisi katika kazi zetu
  7. Urasimu hauvumiliki
  8. Unyenyekevu
  9. Uwazi
  10. Uadilifu
  11. Uzingativu wa ushauri na maonyo
  12. Nidhamu mahali pa kazi
  13. Huduma na ubora wa hali ya juu
  14. Biblia na Katiba ya kanisa ni nguzo za kanisa letu
Kiswahili