Historia
Kanisa la Moravian
lilianza shughuli zake Tanzania mwishoni mwa karne ya 19, ambapo wamisionari
walianzisha kituo cha kwanza Rungwe Kusini mwa Tanzania mwaka 1891. Jimbo la
Kusini-Magharibi lilianzishwa katika mwaka 1976. Jimbo limesajiliwa na Wizara
ya Mambo ya Ndani, lenye namba ya usajili So:6099 na hati yake ya uhalali ni
namba 630. Jimbo hili limegawanyika katika wilaya tatu (3) ambazo ni, Mbeya,
Chunya na Mbalizi. Pia, hufanya utume katika Iringa na Mbozi. Kiujumla jimbo
linafanya maendeleo katika jamii inayoizunguka.
Jimbo linakua kwa
haraka kutokana na idadi ya watu na eneo linalokaliwa. Hili ni jimbo kubwa
zaidi miongoni mwa Majimbo ya Moravian. Limechukua sehemu kubwa ya utawala na
kuleta changamoto za kiusimamizi, lakini jimbo la Kusini-Magharibi (SWP) bado
linajiendesha kwa kutumia jina moja katika mkoa wa Mbeya.
Leo, kuna
wanachama wa Moravian wapatao 215’000 katika jimbo lote, wachungaji na wainjilisti
200 wanaofanya kazi katika shirika 133, na vituo 20 vilivyo mbali na jimbo na Wachungaji wastaafu 25 ambao
wanasaidiwa na jimbo. Asilimia 80 ya bajeti inatokana na vyanzo vyake (Idadi
inatokana na ripoti ya 2019).