Hosteli ya Vijana wa Moravian

Iko katikati ya mji, nyuma ya kituo kuu cha mabasi, Hosteli ya Vijana wa Moravian inatoa huduma kwa wageni wake kwa kuwapeleka kwenye maporomoko ya maji katika eneo la Mbeya, Kusini - Magharibi mwa Tanzania. Mbeya ni mahali pazuri pa matembezi kwa kuona Bonde la ufa Afrika Mashariki. Pia, ni eneo linaloonesha vizuri nyanda za juu Kusini-Magharibi, katika umbali wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (hifadhi ya pili kwa ukubwa Tanzania) na Hifadhi ya Taifa ya Katavi (ni mojawapo ya hifadhi iliyo mbali na haijaendelezwa). Masaa 2 kutoka mpaka wa Zambia - Tanzania na masaa 3.5 kutoka mpaka wa Malawi na Tanzania, Hosteli ya Vijana ya Moravian ni mahali pazuri pa kupumzika na kuburudika.

• Ina vyumba 13 vya kitanda kimoja na vitanda viwili.

Vyumba 6 vyenye choo na bafu

• Ukumbi wa mkutano

• Kikijumuishwa chakula cha asubuhi

• Chakula cha kinyumbani kwa kutoa ombi

• Maegesho ya magari ni bure

• Huduma zinapatikana saa 24

• Muda wa kuingia: 7:00 mchana

• Muda wa kuondoka: saa 4:00 asubuhi

• km 20.3 hadi uwanja wa ndege wa Songwe

Mwelekeo

Hosteli ya Vijana wa Moravian inapatikana katika Ofisi kuu barabara ya Jacaranda, karibu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).


Mawasiliano

Hosteli ya Vijana wa Moravian

S.L.P. 377 
Mbeya
Tanzania

Simu:     +255 755 565 181
      +255 756 772 137Kiswahili