Kituo cha Baraka FM Redio na Studio

BARAKA FM ni kituo cha redio kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini-Magharibi. Kituo cha utangazaji kinapatikana katika eneo la Forest kando ya Mahakama na minara wa kurusha mawimbi ya sauti iko milima ya Kasule  katika mji wa Mbeya.

Kituo kilifunguliwa rasmi mwaka 2008. Msingi mkuu ni kutoa msaada wa kiroho, lakini pia tunatangaza habari na taarifa zingine kwa umma. Baraka FM inaamini kwamba wananchi  wakipewa mwangaza utakuwa msingi wa maendeleo ya ujenzi wa Taifa.

Wakati wa usajili wake katika Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) mwaka 2008, kituo cha redio kiliajiri watu watano na walifanya kazi ndani ya eneo la kilometa zipatazo 42 wakati huo eneo lilikuwa na 60% ya wakazi huko Mbeya. Kwa jitihada, na michango iliyotolewa na serikali na wadau wengine, upatikanaji umeongezeka kutoka kilomita 42 hadi kilomita 200, hivyo, ilituwezesha kuwafikia watu wengi na kuajiri jumla ya watu 16.

Sikilize Baraka FM Redio online:  www.barakafmradio.com !

Upatikanaji wa sasa

Kwa sasa, redio inasikika katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Songwe, Njombe na baadhi ya sehemu za mkoa wa Iringa na Ruvuma.

Licha ya kumilikiwa na Kanisa la Moravian, makanisa yote mengine, mashirika ya dini, mashirika ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali n.k. yanakaribishwa kutumia kituo chetu cha redio, ikiwa maudhui yanaendana na lengo la kuanzishwa kwa redio hii. Hii yaweza kuwa moja ya sababu inayoifanya redio ya BARAKA FM kusikilizwa zaidi mkoani Mbeya.


Mtazamo

Redio yenye ubora na inayosikika katika nyanda za juu kusini, ambayo inafundisha kuhusu maambukizi mapya ya VVU katika jamii ili kuwa na jamii inayowajibika kwa maendeleo ya Taifa.

Lengo

  1. Kuwapa nafasi wanajamii wa Mbeya na maeneo ya karibu kusikilizwa na kupaza sauti zao kupitia redio hii.
  2. Kuandaa vipindi vya redio vinavyoelimisha, kutoa taarifa na kuburudisha na vinavyohusiana na maisha halisi ya watu.
  3. Kuhamasisha mshikamano wa kijamii miongoni mwa wote.

 

Maadili ya msingi

UKRISTU: Tumekusudia kumtangaza Kristo kwa watu kwa maneno, matendo na mawazo.

UBORA: Tunaendelea kutoa huduma za utangazaji kwa ubora wa hali ya juu kwa wateja wetu (wasikilizaji).

MABADILIKO: Tunaendelea kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na  mabadiliko ya mahitaji ya kiulimwengu.

TAALUMA: Tunazingatia maadili ya kazi na uwazi katika shughuli zetu.

UADILIFU: Tunaendelea kudumisha uadilifu kazini kwa wafanyakazi.

HESHIMA: Tunaheshimu na kuthamini utu wa wateja wetu.

WAJIBU WA KIJAMII: Tumelenga kutoa huduma zinazopatikana muda wote kwa bei rafiki kwa umma.

 

Shughuli zetu

  • Kuelimisha jamii kwa njia ya redio
  • Kuifahamisha jamii kuhusu mambo ya sasa na habari nyingine muhimu
  • Kukosoa mambo yasiyo na tija katika jamii 
  • Kuhubiri neno la Mungu kwa watu wote, kwa wanaomwamini Mungu kwa njia ya nyimbo za injili na wachungaji mbali mbali
  • Pia, tunaiburudisha jamii kwa kuwa ni sehemu ya redio BARAKA
  • Kuwasaidia wasiojiweza na wanaojiweza ambao wanahitaji msaada

Mawasiliano

Ofisi kuu:

Baraka FM
Mahakama Street, Old Forest Area
S.L.P 377
Mbeya
Tanzania

Barua Pepe:
Redio:      fmradiobaraka@gmail.com
Meneja:       amulike.charles@gmail.com
Simu:           +255 762 933 360
       +255 753 900 150
Web:       www.barakafmradio.com

Social Media:
Kiswahili