Msaada wa Kisheria
Kanisa la
Moravian Jimbo la Kusini-Magharibi mwa Tanzania limejifunza kupitia shughuli
zake katika mikoa mingine ya Tanzania kwamba wanawake, watoto na makundi
mengine ya watu waishio katika mazingira magumu mkoani Songwe wanakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa msaada wa kisheria na kukosa uelewa kuhusu haki zao na wapi wanaweza kuzipata
haki zao. Hivyo, tangu mwezi Januari 2017 hadi sasa, Kanisa la Moravian jimbo
Kusini-Magharibi mwa Tanzania, kwa kushirikiana na LSF, limekuwa likifanya kazi
kubwa ya kuwajengea uwezo watu wa vijijini na mijini. Tunalenga kuhakikisha
kwamba elimu ya kisheria na msaada wa kisheria unapatikana na unafikika kwa
watu wote, hasa kwa wanawake. Mradi umelenga katika upatikanaji wa haki kwa
wote, kuhusiana na matatizo ya ardhi, GBV, VAC, migogoro ya wafanya kazi,
urithi, ndoa, kesi za madai na jinai
hasa kwa wanawake mkoani Songwe.
Huduma zetu:
- Utoaji wa huduma halali za kisheria kwa wateja – Wasaidizi wa wanasheria hupokea wateja wenye matatizo ya kisheria, wanawashauri na kutatua migogoro ya kisheria kwa kutumia njia mbadala za usuluhishi wa migogoro. Kesi nyingi hutatuliwa, baadhi zinapelekwa katika mihimili mingine ya haki. Pia, wanasaidia wateja kwa kufuatilia kesi zilizopelekwa katika mahakama za rufaa na kuwashauri wateja wao ipasavyo.
- Utoaji wa elimu ya kisheria na uelewa - Elimu ya jumuiya hutolewa kwa njia mbalimbali, kama baraza la migogoro la kata, vilabu vya shule, sherehe za umma, mikutano ya kijiji, VICOBA, mikutano ya kidini, makundi ya kidini (vikundi vya wanawake), vikundi vya vijana, vikundi vya waimbaji , Makundi ya shule za Jumapili, makundi ya kiinjilisti, mikutano ya wakulima na mingine. Mada zinazojadiliwa wakati wa utoaji wa elimu ya kisheria ni pamoja na masuala ya ardhi, ndoa, GBV, matunzo ya watoto, urithi, haki za wanawake, ujasiriamali, haki za kibinadamu na katiba.
- Mafunzo na
ufuatiliaji wa wasaidizi wa wanasheria
Utawala
Mkurugenzi Mtendaji | Mratibu | Afisa Ufuatiliaji na Tathmini | Mhasibu |
Rev. Willey Mwasile | Nsevilwe Msyaliha | Isabella Kaonga | Mwitishilwa Kalengo |
Mawasiliano
Legal Service Facility - Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania
Barua Pepe: moravainparalegal@gmail.com
Simu: +255 754 516170
+255 763 986859