Idara ya Hospitali na Magereza
Idara ya Gereza na Hospitali ilianzishwa kwa mujibu wa dhana ya kibiblia "nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia." (Mathayo 25:36)
Kazi ya mchungaji wazamu ni kuhubiri injili, kuombea wagonjwa na kutoa ushauri nasaha kwa wafungwa. Wajibu mwingine wa mchungaji kuwafundisha wafungwa namna ya kujitegemea. Mara baada ya kuwa huru, waweze kufanya kazi wenyewe. Kazi ya tatu kuwasaidia wafungwa kwa kuwapa nguo, sabuni, bidhaa za usafi, Biblia na vitabu vya nyimbo.
Huduma hii hutolewa
na jimbo ilianza mwaka 1999, na wachungaji wa sasa ni Mch. Stephano Ngondya
aliyehudumu miaka 14 na Mch. Ambukege Mwaihoba.
Magereza yanayohudumiwa na wachungaji ni:
- Songwe (wafungwa 357)
- Ilembo (wafungwa 270)
- Mbalali (wafungwa 102)
- Ngwala (wafungwa 65)
- Ruanda (wafungwa 1500)
- Mkwajuni
(wafungwa 20)
Mafanikio
Injili ya
Yesu imekuwa ikihubiriwa kwa wafungwa, ambapo watu wa dini nyingine
wamebadilishwa na kuwa Wakristo.
Changamoto
- Wafungwa hawana mablanketi ya kutosha, mashuka, sabuni na Biblia.
- Ukosefu wa usafiri kwa wachungaji walio zamu. Njia nzuri ya usafiri inabidi liwepo gari.
- Umbali wa kwenda magereza, kwa mfano gereza la
Nguala ni kilomita 258 kutoka Mbeya.
Matarajio
Matarajio
yetu kuhakikisha kwamba wafungwa wanakuwa raia wema, na kulitumikia Taifa na
kanisa pia.
Mapendekezo
Tunapendekeza
kwamba Wakristo watoe msaada kwa wafungwa kama vile nguo, viatu, mablanketi,
sabuni na bidhaa za usafi
Mawasiliano
Kanisa
la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Idara ya Gereza na Hospitali
Mbeya
Tanzania
Simu: +255 752 334625