Idara ya Wanawake na Watoto

Idara ya Wanawake na Watoto ya Kanisa la Moravian – jimbo la Kusini-Magharibi ina jukumu la kusaidia jamii. Inasaidia wanawake na watoto na dai haki zao katika jamii. Kwa kukabiliana na idadi kubwa ya watoto yatima na watoto wenye maisha magumu, hasa kutokana na maambukizi ya VVU / UKIMWI, kanisa lilianzisha mradi wa watoto yatima na watoto wenye maisha magumu huko Nsalaga. Ili kupata taarifa zaidi juu ya mradi huu, bofya linki ya chini.

Mradi wa Watoto Yatima na wenye maisha magumu - Nsalaga


Umoja wa Wanawake na Uwezeshaji

Amani, upendo na mshikamano ni maneno muhimil wa idara ya Wanawake na Watoto. Wanawake wa Tanzania wanakabiliwa na ubaguzi wa kijinsia, hasa katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania. Inaaminika kwamba hii ni kutokana na ukosefu wa maarifa. Wanawake hawa wanafanya kazi ya kubadilisha mila mabaya za kitamaduni zihusuzo masuala ya kijinsia na kuleta usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake. Wanasema kwamba mwanamke anapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa kama wanaume walivyo. Wanawake wanapaswa kupata elimu bora, nafasi za uongozi na ufundishaji. Wanawake lazima wapiganie uhuru wao kiroho, kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Ili kukabiliana na mambo hayo, Idara ya Wanawake na Watoto imeanzisha miradi ya kupiga vita mimba za utotoni, ndoa za utotoni na idadi kubwa ya vifo kwa kuunga mkono elimu kwa wasichana. Hata hivyo, idara hiyo inawezesha wanawake na wasichana sio tu kwa kuwasaidia kulipa ada za shule na mahitaji ya msingi ya shule, lakini pia kwa kuwafundisha jinsi ya kupata kipato na kujitegemea kiuchumi. Mfano mmojawapo, ni warsha za ushonaji na ufumaji ambazo zinaandaliwa na idara. Kwa ujuzi huu, wanawake wanaweza kufanya kazi wakiwa nyumbani na kujipatia kipato cha ziada kwa ajili yao na familia zao.

Idara pia inaandaa kozi za uongozi, mafunzo ya kompyuta, ujuzi wa ujasiriamali na Kiingereza. Viongozi wanawake hufundishwa wakati wa warsha, baada ya mafunzo hurudi shirikani na kuelimisha wengine kwa ujuzi walioupata. Kwa njia hii, wanawake wanaoishi katika maeneo ya mbali wanaweza kufikiwa, kushauriwa na kuwezeshwa. Pia idara ilianzisha vikundi vya akiba na mikopo (VICOBA), kusaidia wanawake wapate mikopo midogo ili waanzishe biashara na kuendesha miradi yao.

Zaidi ya hayo, Idara ya Wanawake na Watoto inaandaa semina juu ya afya ya akili, inayoitwa CPE (clinical pastoral education), kuwasaidia wanawake wenye hali ngumu na kuwasaidia kiakili. Wanawake wa Kanisa la Moravian pia huwasaidia wanawake walio na maisha magumu na watoto wao wanaoishi na maambukizi ya VVU, saratani na ugonjwa wa kisukari. Katika semina, wajane hupata mafunzo na kuelimishwa kuhusu haki zao za kibinadamu na matatizo yahusuyo jinsia. Wanawake pia hutoa msaada kwa wagonjwa, kuwatembelea hospitalini au gerezani na kuhudhuria mazishi. Pia kuna wanawake wengi wenye matatizo mbali mbali. Hivyo, kuwaombea, kuwasikiliza na kuwaunga mkono ni muhimu katika kuleta mafanikio.

Wanawake hukutana kwa pamoja kila Jumatano na Ijumaa kwa ajili ya kuombea familia zao, viongozi, shule, makanisa na Taifa. Pia hukusanyika siku maalum kama vile siku ya Baraza la Makanisa Tanzania (Siku ya CCT), Siku ya maombezi ya Wanawake duniani, Siku ya Watoto, Siku ya yatima, na Siku ya Wamoravian (Siku ya MCT). Ni wakati huu wanawake wanapewa fursa ya kusali pamoja na kuchangia fedha za kusaidia miradi ya kijamii, katika jimbo na shirika.

Mwisho, Idara ya Wanawake inawajibika na walimu wa shule ya Jumapili katika shirika 198, ambapo kuna walimu wa shule za Jumapili kadhaa katika kila usharika. Wanaandaa warsha, kutoa mafunzo na msaada kwao katika kazi zao. Kwa mfano, kutoa maarifa bora juu ya elimu na saikolojia watoto.


DARASA LA UFUMAJI NA USHONAJI
A. Historia fupi
Idara ya Umoja wa Wanawake na Watoto pia inaendesha darasa la ufumaji na ushonaji kwa ajili ya wanawake na wasichana. Darasa hii lilianza Januari, 2018. Darasa limefadhiliwa na shirika la Mission 21 chini ya uongozi wa Adrianne Sweetman. Wanawake wote wa KMT-JKM na wasio wa moravian wanakaribishwa kuhudhuria darasa hili ili kuboresha maisha yao ya kila siku. Darasa lipo Makao Makuu ya kanisa Jacaranda.

Malengo ya darasa ni:
  • Kuboresha maisha miongoni mwa wanawake
  • Kuwafanya wanawake wajitegemee
  • Kuinua maendeleo ya kiuchumi ya jimbo
B. Awamu
1. Januari - Machi, 2018 waliohitimu walikuwa ..............
2. Aprili - Juni, 2018 waliohitimu walikuwa  29
3. Julai - Septemba, 2018 waliohitimu walikuwa 26
4. Oktoba - Disemba, 2018 waliohitimu walikuwa ..................
5. Januari - Machi, 2019 waliohitimu walikuwa ..............
6. Aprili - Juni, 2019 waliohitimu walikuwa 19 wamama 02 na wasichana 17

C. Watumishi
1. Salome Mnkondya anahusika na ufumaji
2. Tukulamba Mwakanyemba anahusika na ushonaji
3. Jenipha Kamendu anahusika pia na ushonaji

D.  Matarajio ya Baadaye
(a) Mbozi - Vwawa Mkoa wa Songwe
(b) Ilembo katika Wilaya ya Mbeya Vijijini
(c) Mbarali
(d) Chunya

Mkuu wa Idara - Tulinagwe Kibona
Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Idara ya Umoja wa Wanawake na Watoto

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Simu:    +255 755 987288
Barua Pepe:  tulinagwekibona@gmail.com

Kiswahili