Ofisi ya Mkaguzi wa ndani

Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani inafanya huduma za uhakikisho, kufuatilia udhibiti wa ndani, kukagua na kuchunguza mfumo wa fedha na uendeshaji, kukagua kama sera za udhibiti wa ndani zinafuatwa, kanuni na udhibiti wa kanisa na sheria za nchi, kupitia taratibu utawala na uendeshaji kama zinafuatwa.  

Majukumu ya Mkaguzi wa Ndani. 

(a) Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa upokeaji, uhifadhi na matumizi ya rasilimali zote fedha na watu;

(b) Kupitia na kutoa taarifa juu ya ufuasi wa taratibu za fedha na uendeshaji zilizowekwa katika sheria yoyote au kanuni au maelekezo yoyote yaliyotolewa chini ya sheria hiyo na utaratibu mzuri wa uhasibu kama inavyofafanuliwa na taratibu za fedha, mara kwa mara na kuidhinisha malipo kwa kiwango ambacho kingehakikisha ufanisi.

(c) Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uainishaji na mgawanyo sahihi wa hesabu za mapato na matumizi;

(d) Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uaminifu na uadilifu wa data za fedha na uendeshaji ili taarifa zinazotolewa ziruhusu utayarishaji wa taarifa sahihi za fedha na ripoti nyinginezo kwa taarifa za umma kwa ujumla kama inavyotakiwa na sheria.

(e) Kupitia na kutoa ripoti kuhusu mifumo iliyopo inayotumika kulinda mali na uhakiki wa kuwepo kwa mali hizo;

(f) Kupitia na kutoa ripoti kuhusu utendakazi au programu ili kubaini kama matokeo yanawiana na malengo yaliyowekwa;

(g) Kupitia na kutoa taarifa kuhusu utoshelevu wa hatua za menejimenti katika kujibu ripoti za ukaguzi wa ndani, na kusaidia usimamizi katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti hizo na pia, inapobidi, mapendekezo yaliyotolewa na mkaguzi wa nje.

(h) Kupitia na kutoa taarifa juu ya utoshelevu wa udhibiti uliojengwa katika mifumo ya kompyuta inayotumika katika jimbo.


Ndg.  Jairi P. Mwasegile - Mkaguzi wa ndani KMT-JKM

Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzanoa Jimbo la Kusini Magharibi
S.L.P 377
Mbeya.

Simu: +255754 057738
Email: jmwasegile1@gmail.com 
Kiswahili