Idara ya Vijana

Historia

Hapo mwanzo, idara hii iliitwa “Idara ya Vijana na shule ya Jumapili”. Shule ya Jumapili ilianzishwa na Robert Raikes kwa lengo la kufundisha watoto maskini kusoma, kuandika na kujifunza neno la Mungu. 

Mwaka 1844, Bw. George William alikusanya vijana katika viwanda ili kuwafundisha neno la Mungu. Baadaye alilipa jina shirika la vijana "Young Men Christian Association” (YMCA). Mwaka 1861, Sr. Emma Kinnard alianzisha umoja wa wanawake ulioitwa "Young Women Christian Association” (YWCA) kwa lengo la kuimba, kupiga kinanda na kufanya kazi za nyumba. Mwaka 1875, hivi vyama viwili vilijiunga na kuwa kundi moja. Mwaka 1959, chama hicho kiliingia Tanganyika na kiliitwa "Young Christian Association” (YCA).

Kanisa la Moravian liliikubali taasisi hii kama mwanachama wake mwaka 1958 katika Sinodi ya Msangano Mbozi. Wakati huo, ofisi kuu ilikuwapo Rungwe na majimbo mawili (Jimbo la Kusini na jimbo la Kusini-Magharibi) yalikuwa hayajagawanywa. Taasisi ilikuwa kitengo cha "Vijana" chini ya Idara ya Elimu ya Kikristo mwaka 1976 na kuzaliwa kwa Kanisa la Moravian nchini Tanzania jimbo la Kusini-Magharibi.


Malengo

Kitengo cha Vijana kimegawanyika katika sehemu mbili. Kundi la kwanza linaitwa Vijana A na lina vijana kati ya umri wa miaka 13 na 25. Kundi la pili linaitwa Vijana B na lina watu wenye umri wa miaka 26 hadi 45 na watu wote walioolewa au kuoa (bila kujali umri).

Lengo I: kuandaa vijana kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wao na kueneza injili.

Lengo la II: kuendeleza mizizi ya maisha ya kiroho kwa vijana kwa njia ya ibada na masomo ya Biblia (binafsi na katika vikundi).

Lengo la III: kuendeleza umoja kati ya vijana katika Kanisa la Unitas Fratrum na kushirikiana na vijana wa makanisa mengine ndani na nje ya nchi.

Lengo la IV: kuhamasisha vijana kuwa waaminifu, kuwafundisha kuhusu uongozi wa Kikristo, na kukua na kuendeleza Ukristo maishani mwao.

Lengo V: kuwahimiza na kuwaruhusu vijana kufurahia muziki, michezo na maigizo.

Lengo la VI: kuwa na haki ya kuimba ibadani kama kundi kanisani.

Lengo la VII: kuwasaidia vijana wajitegemee kiuchumi.

Idara hii kwa sasa inaongozwa na Mch. Amos Chiwila Mwampamba
Mawasiliano: +255 755 148 514
Kiswahili