Mipango ya Uchumi na Maendeleo

Idara ya Mipango ya Uchumi na Maendeleo, inaandaa na kusimamia miradi mingi katika jimbo. Lengo ni kupambana dhidi ya uharibifu wa mazingira, kuongeza mapato ya jimbo na kupunguza umasikini wa waumini wa Kikristo wa Moravian. Idara inaendeshwa na Mch. Nsevilwe Msyaliha akisaidiana na Ndugu Essau Swilla kama Meneja wa Miradi katika Jimbo.

Shughuli nyingine ya Idara ni kuandaa semina juu ya maendeleo ya kiuchumi kwa idara mbali mbali na kukuza uwezo wa kujijenga ndani ya kanisa.


Mtazamo

Kuinua mapato ya jimbo na kupunguza umasikini kati ya jimbo na waumini wake.

Lengo

Kuchangia uboreshaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jimbo.Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Mipango ya Uchumi na Maendeleo

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Simu: +255 763 986 859                                                                                          Mch. Nsevilwe Msyaliha
Barua Pepe:   
Kiswahili