Dawati la VVU

VVU / UKIMWI ni ugonjwa usio na ubaguzi na unadhoofisha, uko katika sekta zote. Ni mojawapo ya matatizo katika jamii ya Kitanzania, kila idara na taasisi ya Kanisa la Moravian linaguswa nalo. Miradi mbalimbali inatekelezwa ili kuzuia, kujali na kupunguza unyanyapaa.

Mwanzoni mwa mwaka 2012, ofisi ya uratibu ilianzishwa ili kuratibu miradi mbalimbali inayohusiana na VVU / UKIMWI na kuhakikisha kwamba jitihada hizo hazirudiwi. Mwaka 2015, ilikuwa idara hai iliyoitwa Dawati la VVU, yenye lengo kuu la kusaidia jamii kupunguza kiwango cha maambukizi mapya kwa kizazi kisicho na VVU. Tangu kuanzishwa kwake, kanisa limekuwa likishirikiana na serikali ya Tanzania, Mission 21 na wadau wengine ili kuhakikisha kunapunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa asilimia 90.

Dawati la VVU linafanya kazi katika mikoa ya Mbeya na Songwe na linashughulikia wilaya nne, yaani: Mbeya DC, Chunya, Mbozi na Momba.

Malengo makuu ya Dawati la VVU ni:

  • Kuzuia maambukizi mapya

  • Kuwasaidia  watu walio na VVU / UKIMWI

  • Kupunguza unyanyapaa katika jamii

Tunayafanyia kazi malengo haya kwa njia mbali mbali. Kwa mfano, kwa kutoa ushauri nasaha na upimaji, hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa. Ni muhimu kuzuia ueneaji wa ugonjwa huo. Pia tulianzisha vilabu katika shule zetu na vyuo, kuongeza ufahamu na kuwajulisha wanafunzi kuhusu maambukizi ya VVU / UKIMWI. Zaidi ya hayo, tunafanya kazi na “Community Based Health Supportes” (CBHS). Hawa ni watu wanaojitolea ambao hufanya kazi katika jumuiya na kutoa elimu ya VVU na kuwatembelea watu walioathiriwa na VVU katika nyumba zao. Tunafanya kazi pamoja na waelimishaji wa rika, ambao huchaguliwa na kanisa na husaidia kanisa kutoa elimu kwa wenzao katika jamii (ToT). Mbali na elimu kwa njia ya rika sawa na CBHS, tunaandaa vipindi vya redioni katika Baraka FM ili kuelimisha idadi kubwa ya watu. Zaidi ya hayo, tulisaidia kuundwa kwa vikundi vya kujihudumia, ambapo watu walioathiriwa na VVU / UKIMWI wanaweza kuzungumza juu ya matatizo yao na kubadilishana mawazo ya namna ya kuishi na ugonjwa huo. Baadhi ya vikundi hivyo vilianzisha vikundi vya akiba na mikopo (VICOBA), ambavyo vinawasaidia kufadhili miradi yao ili waweze kuzalisha kipato na kuishi maisha mazuri na kupata chakula bora. Kwa sasa, tunafanya kazi na hivyo vikundi  sita vya kujihudumia, kila kimoja kina watu 25.

Mradi unafanya kazi na mtumishi mmoja wa programu, wasaidizi wa Afya wa Jamii 15 (CBHS) na waelimishaji rika 60 kutoka kwenye maeneo lengwa.


Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Dawati la VVU

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Barua Pepe: isabelakaonga@yahoo.com
Simu:       +255 763 439712
Kiswahili